Wednesday, June 24, 2009

KWA MARA NYINGINE!!!!

Sasa sijui inakuwaje jamani,Top In Dar,Khaleed Mohamed inasemekana kampiga mtu kwa mara nyingine,amempiga mwanafunzi ukumbini na kutokwa na damu kichwani na mdomoni na tayari amesharipoti polisi,duhhh cjui wadau tusubiri kitakachofuata.

Monday, June 22, 2009

NIKO KATIKA KIPINDI CHA KIJANJA!







Nilipata bahati ya kuingia katika kipindi cha kijanja THE SPLASH ila mhhh nilishika nafasi ya Mtoto wa mjengoni,Agnes Anderson ambaye hakuwepo kuikamata baada ya kufiwa na Aunt yake,ila nilikamata kisawasawa mpaka mwenye usukani wake Baba wawili Edwin Bashir alisaliti amri.



Wednesday, June 17, 2009

HALI BADO NI MBAYA TUENDELEE KUMUOMBEA!!!!!



KIPENZI CHA WATU,MWALIMU WA WALIMU,GENERALI BANZA STONE JAMANI HALI YAKE BADI NI TETE,JAPO AMETOKA HOSPITALI LAKINI KWA MUJIOBU WA NDUGU ZAKE NI KWAMBA HALI YAKE JAMANI BADO NI MBAYA SANA HAIKO TOFAUTI NA ILEILE YA AWALI ALOPOKUWA AMELAZWA,JAMANI WADAU MMHHHH TUENDELEE KUMUOMBEA!

YASIJE TOKEA YA TANDALE....!


Jamani jamani taratibu yasijetokea ya huko Tandale ya wale wapenzi wawli wawili hivi majuzi walipojikuta wakiwa kwenye wakati mgumu baada ya kumaliza shughuli zao za kimapenzi [kujamiiana] kushindwa kuachiana baada ya jibaba kushindwa kutoa nyeti zake kutoka kwenye nyeti za mpenzi wake.
Maana nao walipanga miadi ya kukutana katika nyumba moja ya kulala wageni hukohuko Tandale na wakiwa wanamaliza kupeana maraha,malavidavi,kupeana mahabati,makuchukuchu hotahe kama kawaida jamaa akawa anataka kutoa nje kitu yake na kujikuta hakitoki.
Jamaa ikawa kila akijitahidi kuutoa na kutumia kila aina ya ujanja wake alishindwa kujinasua kwa mwanamke huyo na kuamua kuchukua umamuzi wa kupiga kelele ili wahudumu waingie waje kumnasua lakini nao pia walishindwa na kuwalazimu kutoa taarifa katika kituo cha polisi na kusababisha watu kujaa na kuwashuhudia live .......wakiwa katika libeneke hilo.
Jamani wake za watu na waume za watu nisumuuuu!

SIJUI NITAKUJA VIPI LEO KATIKA JAMBO BEAT!


Bonnie Obama,Bonnie Sly,Mzee wa kuvuta Pumzi leo hiyo kama akitafakari atakuja vipi leo katika kuimalizia Historia ya Koffie ndani ya jambo beat ya Ebony Fm na Bahati Alex katika segment yake ya Jambo Celebritie's.

KWA USAFI JAMANI MMMhhhhh!


















Mdau sijui we waonaje lakiniii?Ni hospitali yetu mkoani Iringa



Tuesday, June 16, 2009

KWA NAZIIIIIII.....!



IRINGA NASI TUMO JAMANI SAMAKI WA MTERA WAMEJAA TELE,HAWA NI WALE WAKAVU KUWAPIKA MPAKA UWATUMBUKIZE KATIKA MAJI YA MOTO KWANZA,BASI UKIWATIA BAMIA KIDOGO,NYANYA CHUNGU KIDOGO TWAITA NYANYA CHNGU ZA KUTUPIA UKIPATA NA NAZIIII ROJO LIKWA ZITOOO KWA UGALI AHAAAA UMEFIKA MAHALA PAKE....!

JAMANI MBONA KAMA AMEOKO......!


Wadau nisaidie jamani huyu jamaa mbona kama hicho alichoshika mkononi amekitoa katika huo mfuko aliotupa matakataka......sijui unaonaje nisaodie miye!

Monday, June 15, 2009

Jambo Beat ya leo ilikuwa poa!




Nikiangaza angaza angalau kupata kidogo mwanga wa jua baada ya kukaa studio saa 3 kuanzia 4asb mpk 7mchn katika Jambo Beat,leo ilikuwa poa maana Bonnie Obama alinifurahisha sana na Historia ya Koffie Olomide japo aliniachia na hamu ya kutaka kujua mengi zaidi juu yake lakini sikutia shaka kwa kuwa najua panapo majaaliwa kesho atatupa muendelezo,agape naye leo katika kurasa za moto mmmmhhh kuna moja ilikuwa kali ya jamaa aliyemkata mwenzie nyeti zake baada ya kumfumania na mkewe basi alimradi raha tupu ndani ya Jambo Beat leo.

Bonnie Obama leo Katika Jambo beat

Wiki yote iliyopita jamaa katika segment yake ya Jambo Celebrities ndani ya Jambo Beat alikuwa akitupa uhondo wa wale mapacha wawili kutoka hukoooo Nigeria nawazungumzia Petter na Paul Okoye wewe umezoea kuwaita P square,leo jamaa anaanza naye Koffie Charles Olomide,tutamfahamu kiundani hasa wapi kazaliwa,vipi elimu yake na kazi za muziki alianza lini na mengine mengi usiyoyajua kuhusu huyo bwana mkubwa,mkamate Bonnie Obama leo kunako saa 5 ndani ya Jambo Beat ya Ebony fm.

AGAPE WA MSUMARI

Anaitwa Agape wa Msumari anarindima naye katika Jambo Beat ya B1 ndani ya Ebony Fm yupo katika segment yaitwa kurasa za moto,wallah kama za moto na anapozisomo huwa zinaunguza kabisaaaaa mkamate kunako saa 4.40 asb akiwa na B1.

Friday, June 12, 2009

GARI YA MANENO,4 BY 4

Anaitwa Hatya Omary,Mamaa Sinyorita,Mwarabu wa Dabaga,Gari ya maneno,Medeshee kubwa,4 by 4 yote hayo ni majina yake,yupo naye ndani ya jambo Beat ya Bahati Alex kunako saa 4asb mpaka saa 7mchana ndani ya Ebony Fm,yeye anaingia kwa dakika takriban 7 tu lakini wallah si mchezo atakupa vijimambo vilivyojaa mambo

Thursday, June 11, 2009

BONNIE OBAMA


Anaitwa Bonnie Zakaria au Bonnie Sly,yupo katika Jambo Beat ya Ebony fm naye akifanya mchakato wa kutupa historia za watu maarufu duniani,mpate kunako saa 5 asb na moja ya hiyo segment yake.

B 1, B SINGLE, B WA KWANZA, B ORIGINAL.

Helo helooooo, mashostito ndo hivyo tena nshagonga hodi bloguni, zile raha na utamu ulozoea kuupata radioni sasa umeingia mtandaoni. wengi walio nje ya nchi wameniomba sana na sasa ndo nshayavulia nguo haya maji mie na nyie, libeneke ndo limeanza. halooooo